COVID-19

Asthma (Swahili)

AACALD2020_Swahili_10 Ways to Live Well

AACALD2020_Swahili_Asthma Action Plan

AACALD2020_Swahili_What your doctor needs to know

SWAHILI ENGLISH
Virusi vya Korona ni familia ya virusi ambavyo hufanya watu kuumwa, kama vile homa za kawaida na maambukizo mengine ya njia ya juu ya kupumua. Coronaviruses are a family of viruses that make people sick, such as common colds and other upper respiratory tract infections.
COVID-19 ni aina ya virusi vya korona ambavyo husababisha watu wengi kuwa wagonjwa na kukuza ugonjwa mbaya zaidi kuliko magonjwa mengine ya virusi vya korona. COVID-19 is a kind of coronavirus which is causing more people to be sick and develop more serious illness than other coronaviruses.
Hakuna namba maalum bado ya kupendekeza kwamba watu walio na ugonjwa wa pumu wako katika hatari kubwa ya kupata virusi. Wala hakuna ushahidi wowote kupendekeza kwamba watu walio na pumu wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa mbaya zaidi ikiwa wataupata. There is no specific data as yet to suggest that people with asthma are at a higher risk of contracting the virus. Nor is there any evidence to suggest that people with asthma have a higher risk of experiencing serious illness if they get it.
Lakini tunawahimiza watu wenye ugonjwa wa pumu na familia zao na jamii kufanya kila wawezalo kujilinda wenyewe na wengine. But we encourage people with asthma and their families and communities to do everything they can to protect themselves and others.
Mojawapo ya mambo mazuri unayoweza kufanya kupunguza hatari yako ni kuongeza udhibiti wa ugonjwa wa pumu yako na kuwa na afya nzuri. Hii ni pamoja na kusimamia hali zingine za muda mrefu na kuzingatia kula kwa afya vizuri, mazoezi na kudhibiti mafadhaiko yako. One of the best things you can do to reduce your risk is to optimise your asthma control and stay healthy. This includes managing other long-term conditions and focusing on eating healthy, exercising and managing your stress.
Inapokuja suala la kudhibiti ugonjwa wa pumu yako, fikiria orodha ifuatayo: When it comes to managing your asthma, consider the following checklist:
AACALD2020_Swahili_10 Ways to Live Well
Kumbuka: Watu wenye ugonjwa wa pumu wanapaswa kuendelea kutumia dawa za kuzuia ugonjwa wa pumu kama inavyoamriwa. Note: People with asthma should continue to use their inhaled asthma preventer medications as prescribed.
Vyanzo vingine vimependekeza kwamba uache kutumia vidonge vya pumu “corticosteroids” wakati wa janga la COVID-19. Lakini habari hii ni ya watu kwa ujumla na haielekezwi kwa watu walio na ugonjwa wa pumu ambao wanahitaji kuchukua dawa yap umu za corticosteroid kusimamia hali zao au kutibu ugonjwa wa pumu (shambulio). Some sources have recommended that you stop taking “corticosteroids” during the COVID-19 epidemic. But this information is for the general population and is not directed at people with asthma who need to take corticosteroid medication to manage their condition or treat asthma flare-ups (attacks).